Makonda atumia Mil 24 kuwatuza wachezaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Jun 2019
Makonda atumia Mil 24 kuwatuza wachezaji Simba

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda leo ametimiza ahadi ya kuwatunza wachezaji wote wa Simba walioibuka na tuzo kwenye hafla ya Mo Simba Awards lililofanyika mwishoni mwa wiki Kilimanjaro Hotel jijini Dar es salaam

Makonda ambaye ni mdau mkubwa wa klabu ya Simba amesema zawadi hizo ni sehemu ya kutambua mchango wao lakini pia ni hamasa kufuatia ubingwa wa ligi kuu waliotwaa pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa kufika hatua ya robo fainali

Amewataka wachezaji hao kutumia fedha hizo kuanzisha miradi ya maendeleo itakayowasaidia kuingiza kipato pindi watakapostaafu mpira huku akiwataka kutumia umaarufu na Brand zao kujiingizia kipato

Waliopata zawadi hizo ni wachezaji wote waliotwaa tuzo Mo Simba Awards wakiongozwa na mlinda lango Aishi Manula ambaye yeye alipata Tsh Milioni 10 ikiwa ni ahadi aliyoitoa Makonda mapema kwa mlinda lango huyo wakati wa michuano ya ligi ya mabingwa

cut

Wengine ni Meddie Kagere, Rashid Juma, John Bocco, Erasto Nyoni, Clatous Chama na James Kotei

Mwanahamisi Omary Shurua, mchezaji bora wa kike alipata Milioni mbili na msemaji wa Simba Haji Manara amepatiwa milioni tatu kama sehemu ya kutambua mchango wake kwenye uhamasishaji

Makonda amewataka wachezaji kuchukulia michezo kama pesa, uchumi, amani na biashara inayoweza kuwafanya wao binafsi wanufaike kiuchumi na taifa lipate mapato ya kutosha kupitia mapato yanayoenda kwenye manispaa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’