Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ameonyesha kuwa na imani kubwa kwa beki wa kulia wa Simba, mabingwa wa Tanzani Bara Shomari Kapombe ambaye alimjumuisha kwenye kikosi chake kinachojiandaa na fainali za AFCON 2019 licha ya beki huyo kuwa nje kwa zaidi ya miezi mitano kutokana na majeraha ya goti
Hata hivyo inaelezwa Kapombe anaweza asiwe sehemu ya wachezaji watakaoelekea Misri kushiriki michuano hiyo baada ya kujitonesha jeraha kwenye mazoezi ya Stars yanayofanyika uwanja wa Taifa

Kwa sasa Kapombe amepewa program maalum ya mazoezi inayosimamiwa na Madaktari wa Stars na Simba
"Madaktari wamempa program maalum ya mazoezi ili kuona kama anaweza kuwa fiti tayari kwa mashindano," amesema Clifford Ndimbo, msemaji wa TFF
"Hata hivyo kama mambo yatakuwa tofauti taarifa itatolewa"
cutKapombe aliumia mwezi Oktoba mwaka jana akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa Afrika Kusini
Matibabu yake yalifanyika huko huko Afrika Kusini yakichukua zaidi miezi minne
Alianza mazoezi mepesi hivi karibuni, mazoezi ambayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kumfanya arejee dimbani bila madhara
Hii ni mara ya pili Kapombe anakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha
Aliposajiliwa na Simba kutoka Azam Fc alikaa nje kwa zaidi ya miezi sita kabla ya kuanza kuwatumikia mabingwa hao wa nchi
Kapombe anatajwa kuwa beki bora wa kulia Tanzania kwa sasa