Niyonzima asubiri mazungumzo ya mkataba mpya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Jun 2019
Niyonzima asubiri mazungumzo ya mkataba mpya Simba

Kiungo fundi wa Simba Haruna Niyonzima ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao ya kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara imemalizika lakini bado mazungumzo ya mkataba mpya hayajafanyika, imefahamika

Niyonzima aliyetua Simba misimu miwili iliyopita akitokea Yanga, alianza maisha yake Msimbazi kwa kusuasua akikaa nje ya dimba mda mrefu kutokana na majeraha na mgogoro wa mkataba wake

Hata hivyo Niyonzima alimaliza msimu vizuri hali iliyopelekea amshawishi Patrick Aussems, Mkufunzi wa Simba ambaye aliagiza aongezwe mkataba

Inaelezwa moja ya sababu inayochelewesha mkataba wa Niyonzima ni dau kubwa la usajili analotaka

Hata hivyo Niyonzima amesema ana matumaini ataendelea kubaki Simba kwa kuongeza mkataba mwingine

"Ningependa kuendela kubaki hapa Tanzania na hasahasa kucheza hapa Simba kwani naamini ni sehemu pekee ambayo naweza kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa wa Afrika," amesema

"Lakini uamuzi uko kwa viongozi wa Simba. Tayari nina ofa kutoka timu nyingine, kama watachelewa kunipa mkataba basi nitafanya uamuzi ambao utakuwa na manufaa kwangu"

cut

Inaelezwa Simba iko kwenye mazungumzo na wachezaji watatu wa kigeni ambao wameletwa nchini na Wakala Patrick Gakumba aliyefanikisha usajili wa Meddie Kagere

Simba ina wachezaji 10 wa kigeni na italazimika kuwaacha baadhi ya wachezaji ili kuongeza wapya

Gharama ya mkataba wa Niyonzima inaweza kuwa sababu ya kiungo huyo kutoongezwa mkataba

Asante Kwasi, Nicholas Gyan na Zana Coulibaly nao wako hatarini wakati Mganda Juuko Murshidi yeye tayari ameondoka baada ya mkataba wake kumalizika

Aidha, mshambuliaji Emmanuel Okwi yeye amegoma kusaini mkataba mpya akiomba kujipanga na atafanya uamuzi baada ya mishuano ya AFCON 2019 inayoanza Juni 21 nchini Misri

Okwi anahusishwa na timu kadhaa za ligi kuu ya Afrika Kusini

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’