Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamewasili salama jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Morogoro ambako walikabidhiwa ubingwa wa ligi kuu jana
Simba ilipokelewa Dar na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ambaye ni mdau mkubwa wa timu hiyo
Shamrashamra za ubingwa zilianzia mkoani Morogoro jana
Simba iliondoka mkoani humo asubuhi ya leo na ilipokelewa wilayani Kibaha kuwapa fursa wakazi wa mkoani Pwani kufurahia ubingwa na timu yao
Baadae Simba iliendelea na safari ya kuelekea jijini Dar es salaam ambapo njiani Wanamsimbazi walijitokeza kwa wingi barabarani kuwalaki mabingwa hao mara mbili mfululizo ligi kuu ya Tanzania Bara
Shamrashamra za ubingwa zimehitimishwa Makao Makuu ya Simba Mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam ambapo wakazi wa jijini Dar es wamejitokeza kwa wingi kusherehekea ubingwa huo
Picha za matukio mbalimbali baada ya Simba kuwasili jijini Dar es salaam;








