Msemaji wa Simba Haji Manara amesema kwa sasa timu hiyo haijafanya mazungumzo na kiungo Ibrahim Ajib anayehusishwa kurejea Msimbazi kwa ajili ya msimu ujao
Manara amesema jukumu la usajili liko chini ya kocha Patrick Aussems hivyo ni yeye mwenye uamuzi wa mwisho juu ya mchezaji huyo na wengine ambao watasajiliwa na Simba
"Mpaka sasa hakuna jambo linaloendelea baina ya Simba na Ajib lakini kama Aussems atatuambia anamtaka Ajib basi tutamsajili mara moja," Manara ameiambia eFM
"Sio Ajib tu, Aussems akimtaka mchezaji yeyote Afrika Mashariki na Kati tutamsajili. Kwa sasa tuko vizuri kiuchumi, tunazo fedha za kutosha kumsajili mchezaji yeyote anayetakiwa na benchi la Ufundi"
"Simba ni timu kubwa, hatuhitaji kupitisha bakuli kuchangisha fedha za usajili"
cutAjib alikuwa akihusishwa kutaka kusajiliwa na TP Mazembe hata hivyo usajili wa mchezaji huyo ulikwama baada ya kushindwana maslahi
Inaelezwa tayari Ajib ameshasaini mkataba wa awali kuitumikia Simba, anasubiri mkataba wake na Yanga umalizike ili atangazwe rasmi kuwa mchezaji halali wa Simba