Bosi Simba awashangaa Yanga na 'bakuli' lao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 May 2019
Bosi Simba awashangaa Yanga na 'bakuli' lao

Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema anashangazwa na klabu ya Yanga kujivisha umasikini wakati pesa kibao zinaingia kwenye klabu hiyo.

"Tunaudhamini Tsh. 980m kutoka kwa mdhamini wetu mkuu sawa na Yanga, tunaudhamini wa Simba TV sawa na Yanga TV na tunahaki za matangazo ya television kama klabu nyingine. Ukipiga mahesabu hapo inakaribia Tsh1.4 Billion wanazopata Simba na Yanga."

"Kuna dhana imekuja kwamba Yanga ni masikini sana, si kweli. Sisi tuliwahi kuwa na hali mbaya lakini hatukulia. Kuna wakati TBL walivunja mkataba Simba, tukawa hatuna chochote bora sasa hivi 1.4 Billion inaingia kabla ya viingilio."

"Wakati hatuna kitu, tulichokifanya ni kupandisha wachezaji vijana, hapo wakaanza kucheza kina William Lucian, Singano, Hassan Isihaka, Ndemla, Mkude na wengine kwa sababu tulijua matumizi yetu lazima yawe madogo kulingana na kipato."

"Hatukuomba mitaani, sasa kama Yanga inalalamika hali mbaya Ndanda, Stand, wasemaje? Yanga wanaanza ligi wakiwa na uhakika wa 1.4 Billion."

"Tulichofanya mwaka huu ni kuweka malengo ya kufika hatua ya makundi kwenye ligi ya mabingwa Afrika. Kwa kuingia hatua ya makundi tumepata dola 550,000 kuingia robo fainali ikaongezeka 100,000 kwa hiyo inakuwa dola 650,000."

"Champions League ni pesa, Yanga ilicheza miaka kadhaa mfululizo lakini wanatolewa hawafiki popote wanaangukia Confederation."

"Kwa kucheza Champions League Simba ilikuwa inajaza uwanja, ikawa inavuna fedha kutokana na viingilio karibu Tsh. 900m (kuanzia hatua ya awali hadi robo fainali). Sasa watu wanafikiria mpira ni mchezomchezo."

"Yanga ilikimbia Kagame Cup, sisi tukacheza tukapata Tsh. 50m. Tukacheza mashindano ya mdhamini wetu mkuu tukawa washindi wa tatu tukapata Tsh. 50m, tumepata 50m kutoka kwa mdhamini wetu kutokana na kuingia robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika."

"Sisi wakati tunacheza Champions League watu walijua malengo yetu ni kucheza mpira tu, malengo yetu ni kuingiza pesa. Hivi hamuoni hata vilabu vya Ulaya vinavyopambania Top 4 ili kucheza ligi ya mabingwa? Ni kwa sababu kuna pesa!"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
29m ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
3h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
21h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’