Bocco ataka shangwe la ubingwa lihamishiwe Morogoro

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 May 2019
Bocco ataka shangwe la ubingwa lihamishiwe Morogoro

Jana mashabiki wa Simba waliojitokeza uwanja wa Taifa kushuhudia 'mnyama' akikabidhiwa kombe baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu, hawakufurahia kuahirishwa kwa hafla hiyo

Licha ya mvua kunyesha, baadhi ya mashabiki walikubali 'kulowana' ili mradi tu washuhudie tukio hilo la kihistoria

Hata hivyo Bodi ya ligi iliahirisha hafla hiyo baada ya mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani Mh Kangi Lugola kupata udhuru

Mtendaji wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura alisema sherehe hizo zimehamishiwa mkoani Morogoro, zitafanyika baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa keshokutwa Jumanne katika uwanja wa Jamhuri

Akingumza baada ya mchezo dhidi ya Biashara United uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, nahodha wa Simba John Bocco aliwashukuru mashabiki waliojitokeza uwanja wa Taifa kuwaunga mkono licha ya hali ya mvua

cut

Amewataka mashabiki hao kuungana na wale wa mkoani Morogoro katika sherehe za ubingwa keshokutwa

Aidha Bocco amewashukuru mashabiki kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya timu hiyo msimu huu

"Kuna wakati tulipoteza mechi, lakini hawakuisusa timu yao, hivyo tulishikamana nao nyakati zote, wanastahili pongezi zote," alisema

"Kulikuwa na viporo vingi, tulicheza mechi nyingi ukichanganya na za kimataifa, lakini tunashukuru tumefikia lengo la ubingwa"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’