Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba itabidi wajilaumu wao wenyewe kwa kushindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Sevilla leo wakiruhusu mabao matatu katika dakika 10 za mwisho na hivyo kukubali kipigo cha mabao 5-4
Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kufunga mabao mawili mapema tu kwenye dakika za 8 na 14 kupitia kwa John Bocco na Meddie Kagere
Sevilla waliouanza mchezo huo taratibu, walipata bao la kwanza kwenye dakika ya 24 kupitia kwa Escudero

Bocco aliyekuwa katika kiwango bora aliifungia Simba bao la tatu kwenye dakika ya 32 akimalizia pasi murua ya Meddie Kagere
Bao la nne la Simba lilifungwa na Clatous Chama kwenye dakika ya 61 akiongeza bao hilo muda mchache baada ya Sevilla kufunga bao la pili kupitia kwa Gil
Mabadiliko ya kikosi kizima yaliyofanywa na kocha Patrick Aussems, yaliiweka Simba kwenye presha kubwa na kujikuta inaruhusu mabao matatu katika dakika 10 za mwisho yakifungwa na Promes (2) na Nolito akifunga la tano kwenye dakika za majeruhi
Licha ya matokeo hayo, Simba ilitoa upinzani mkali kwa mabingwa hao mara tano ligi ya Europa