Mo ataka Bodaboda ziwanufaishe wachezaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 May 2019
Mo ataka Bodaboda ziwanufaishe wachezaji Simba

Ukiachilia mbali zawadi nyingi ambao uongozi wa klabu ya Simba utawapa wachezaji baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo, jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo' aliahidi kuwapa kila mchezaji Bodaboda yenye thamani ya Tsh Mil 2.4

Mo alisema zawadi hiyo itawasaidia wachezaji na familia zao kwani ni kitega uchumi kizuri

"Zawadi hii ya Bodaboda kwa kila mchezaji naitoa mimi mwenyewe. Nimewaambia wachezaji watumie Bodaboda hizo kama kitega uchumi na kuwapa ndugu zao ili kujiingizia kipato kila siku," amesema Mo

"Wanaweza kuingia mikataba na ndugu zao ambao hawana kazi na kujipatia Tsh 15,000/- mpaka pale mikataba hiyo inapomaliza"

"Nimefarijika na mafanikio tuliyopata msimu huu. Umoja na Mshikamano baada ya kuanza uongozi mpya ni chachu ya mafanikio haya"

"Nimethamini kilichofanywa na wachezaji wetu msimu huu ndio maana nimeamua kuwapa zawadi hiyo kila mmoja"

cut

Bilionea huyo amesema msimu ujao wamejipanga kupata mafanikio zaidi ambapo safari hii timu inatarajiwa kwenda kuweka kambi Ureno au Marekani

Simba inatarajiwa kuingia kambini mara tu baada ya kumalizika fainali za michuano ya AFCON 2019 inayofanyika nchini Misri

Wachezaji nane wa kikosi cha Simba wanatarajiwa kushiriki michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’