Mo apongeza ubingwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 May 2019
Mo apongeza ubingwa Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' ameipongeza timu hiyo kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo

Mo amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na juhudi zilizofanywa na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wadau wote wa klabu ya Simba kila mmoja kwa nafasi yake

"Mungu mkubwa. Pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama, mashabiki, na wapenzi wote wa SIMBA, tumeshinda! Najivunia mafanikio haya," amesema Mo

Naye Msemaji wa Simba Haji Manara amewapa shukrani za kipekee wachezaji, benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa timu hiyo kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio ya Simba msimu huu

"Tumshukuru Mungu muweza aliyetaka Simba iwe Bingwa tena"

"Tuwapongeze sana Wachezaji wetu wote, Benchi la ufundi chini ya kocha Patrick Aissems, lakini kipekee tuwashukuru nyie Wanachama na Washabiki wetu ambao mimi nnaamini ndio chachu ya huu ubingwa"

"Kwangu shujaa wa kwanza Simba ni Mshabiki wetu, Tunawashukuru sana"

cut

Simba imetwaa ubingwa leo baada ya kuifunga Singida United mabao 2-0

Mabao ya Meddie Kagere na John Bocco yalitosha kuihakikishia Simba ubingwa baada ya kufikisha alama 91 kwenye msimamo wa ligi

Alama hizo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika michezo iliyobaki

Simba imeibuka na ubingwa huku ikiwa na michezo miwili mkononi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’