Kagere akaribia kuvunja rekodi ya mabao ya ligi kuu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 May 2019
Kagere akaribia kuvunja rekodi ya mabao ya ligi kuu

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere anakaribia kuvunja rekodi ya kupachika mabao ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu sasa akiongoza akiwa na mabao 22

Kagere leo atakiongoza kikosi cha Simba kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Singida United, katika mchezo ambao matokeo ya ushindi au hata sare yataipa Simba ubingwa wa pili mfululizo

Mshambuliaji huyo alietua Simba kwa dau la karibu Milioni 200 mwanzoni mwa msimu, anahitaji kufunga mabao manne tu kufikisha mabao 26 na kuifikia rekodi iliyowekwa na Mohammed Hussein 'Mmachinga' mwaka 1998

Kagere yuko katika nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu akiwaacha washindani wake Heritier Makambo na Salim Aiyee kwa tofauti ya mabao sita huku John Bocco na Emmanuel Okwi wakitofautiana nae mabao saba

Hata hivyo mwenyewe amesema rekodi hizo zitakuja akishaisadia Simba kutetea ubingwa

cut

"Bila kuangalia rekodi zilizopo katika kufunga nilianza kujifikiria mwenyewe kuwa Simba ilinisajili ikiwa mabingwa na wanataka kutetea taji, hivyo kama mshambuliaji natakiwa kufunga mabao ili kuirahisishia timu yangu kufikia malengo yake," Kagere amenukuliwa na Mwanaspoti

"Binafsi nataka tutetee ubingwa na kuna kila dalili ya kulitimiza hilo na baada ya hapo nitajifanyia tasmini nimefanya kazi yangu na kufikia yale malengo ya timu kama mshambuliaji ambavyo nilitakiwa kufanya"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’