Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere anakaribia kuvunja rekodi ya kupachika mabao ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu sasa akiongoza akiwa na mabao 22
Kagere leo atakiongoza kikosi cha Simba kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Singida United, katika mchezo ambao matokeo ya ushindi au hata sare yataipa Simba ubingwa wa pili mfululizo
Mshambuliaji huyo alietua Simba kwa dau la karibu Milioni 200 mwanzoni mwa msimu, anahitaji kufunga mabao manne tu kufikisha mabao 26 na kuifikia rekodi iliyowekwa na Mohammed Hussein 'Mmachinga' mwaka 1998
Kagere yuko katika nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha dhahabu akiwaacha washindani wake Heritier Makambo na Salim Aiyee kwa tofauti ya mabao sita huku John Bocco na Emmanuel Okwi wakitofautiana nae mabao saba
Hata hivyo mwenyewe amesema rekodi hizo zitakuja akishaisadia Simba kutetea ubingwa
cut"Bila kuangalia rekodi zilizopo katika kufunga nilianza kujifikiria mwenyewe kuwa Simba ilinisajili ikiwa mabingwa na wanataka kutetea taji, hivyo kama mshambuliaji natakiwa kufunga mabao ili kuirahisishia timu yangu kufikia malengo yake," Kagere amenukuliwa na Mwanaspoti
"Binafsi nataka tutetee ubingwa na kuna kila dalili ya kulitimiza hilo na baada ya hapo nitajifanyia tasmini nimefanya kazi yangu na kufikia yale malengo ya timu kama mshambuliaji ambavyo nilitakiwa kufanya"