Kikosi cha Simba leo kimeweza kuilaza KMC mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
KMC ilianza kupata bao la kuongoza kabla nahodha John Bocco,hajaisawazishia Simba kwenye dakika ya 16.
Ikitandaza kandanda la kuvutia Simba ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa Jonas Sehukawa, ingizo jipya kwenye kikosi cha Simba leo akiweza kufunga kwenye siku yake muhimu ya kujaribiwa.
John Bocco aliifungia Simba bao la tatu dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika na kuihakikishia ushindi mnono katika mchezo huo wa kirafiki.

ADVERTISE HERE