Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wamebakisha alama nne tu kuweza kurudisha ubingwa mtaa wa Msimbazi kwa msimu wa pili mfululizo
Kuhakikisha alama hizo zinapatikana mapema, kikosi cha Simba kimeingia kambini jana kujiandaa na mchezo dhidi ya Ndanda Fc ambao utapigwa Jumapili kwenye uwanja wa Uhuru
Baada ya mchezo huo Simba itaondoka kuelekea mkoani Singida ambako May 21 itachuana na Singida United
Kocha Patrick Aussems amesema wanahitaji kushinda michezo hiyo ili kujihakikishia ubingwa mapema kuondoka na presha ya michezo ya mwishoni mwa msimu
cut"Tunakaribia kufikia malengo ya kutwaa ubingwa, lakini hatuwezi kuanza kusherehekea sasa kwani bado tunapaswa kupata matokeo kwenye baadhi ya michezo," amesema Aussems
"Hatuchezi kutafuta alama nne au tano, tutacheza kushinda michezo yote iliyobaki"
Simba inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama 85, ushindi kwenye mchezo wa kesho utawafanya wafikishe alama 88 na kuhitaji angalau alama moja tu dhidi ya Singida United kuweza kuwa mabingwa
LIcha ya Yanga kuwa na uwezo wa kufikisha alama 89 kama watashinda michezo yao miwili iliyobaki, Simba imefunga mabao mengi ambayo yatawabeba kwenye ubingwa kama timu hizo zitafungana kwa pointi