Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Paschal Wawa wanawania tuzo ya beki bora wa mwaka
Licha ya kutokuwa dimbani kwa muda mrefu, uongozi wa Simba umetambua mchango wa Kapombe na kumuweka miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo

Kabla ya kuumia, Kapombe alikuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba na hakika anastahili kuwekwa kwenye orodha hiyo
Kazi ya Wawa hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa inafahamika
Licha ya kuumia katika mchezo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya TP Mazembe, mchango wake hauwezi kupuuzwa kwenye michuano hiyo ambayo Simba iliweka rekodi
cutNyoni anakuwa bora kila siku. Ukizungumzia usajili bora kuwahi kufanywa na Simba, hutasita kutaja jina la Erasto Nyoni kwani amekuwa na manufaa makubwa kwa mabingwa hao wa Tanzania Bara
Kupiga kura tembelea tovuti rasmi ya MO SIMBA AWARDS kwa kubonyeza HAPA