Bendera kuagwa Jumamosi, kuzikwa Jumapili Korogwe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Dec 2017
Bendera kuagwa Jumamosi, kuzikwa Jumapili Korogwe
Mwili wa kocha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Dk. Joel Nkaya Bendera unatarajiwa kusafirishwa Jumamosi asubuhi kupelekwa nyumbani kwao, Korogwe mkoani Tanga kwa mazishi.

Bendera aliyeiwezesha Tanzania kufuzu fainali pekee za Kombe la soka la Mataifa ya Afrika (AFCON), mwaka 1980 nchini Nigeria, alifariki dunia juzi jioni katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipofikishwa kupatiwa matibabu.

Ratiba ya msiba wa Naibu huyo Waziri wa Michezo wa zamani inasema kwa sasa ndugu na jamaa wanaendelea kukutana nyumbani kwa marehemu, Sinza Dar es Salaam kwa maombolezo ambayo yataendelea hadi Jumamosi Saa 5.00.

Mwili wake utaagwa katika Hospitali ya Lugalo kabla ya kusafirishwa kwenda Korogwe kwa mazishi.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumapili Saa 10.00 jioni baada ya ibada ya kuuombea mwili wa marehemu katika Kanisa la Mtakatifu Michael.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’