Sare dhidi ya Azam Fc haikubadili mipango yetu - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 May 2019
Sare dhidi ya Azam Fc haikubadili mipango yetu - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema licha ya timu yake kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Azam Fc, hakuna kilichobadilika juu ya mpango wa kutetea ubingwa

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya mchezo, Aussems alisema timu yake ilifanya jitihada zote za kusaka ushindi kwenye mchezo huo lakini walikosa bahati

Aidha amekosoa mbinu waliyotumia Azam FC kuwa hawakuwa na lengo la kushinda

"Tumejaribu kila mbinu kuweza kupata ushindi lakini imeshindikana. Sisi tulihitaji kushinda mchezo huu lakini mwenzetu walikuja kusaka alama moja na wameipata," amesema

"Hata hivyo matokeo haya hayabadili chochote katika mipango yetu ya kutetea ubingwa"

Simba imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imefikisha alama 82

Bado hesabu za ubingwa ziko upande wao kwani wanahitaji alama nane tu ili kutawazwa mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo

Simba imebakisha michezo mitano

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’