Manara aomba sapoti ya mashabiki mchezo dhidi ya Azam FC

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 May 2019
Manara aomba sapoti ya mashabiki mchezo dhidi ya Azam FC

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru leo kuiunga mkono timu yao itakayochuana na Azam FC

Manara amesema mchezo dhidi ya Azam hautakuwa mwepesi kwao na hata kwa wapinzani wao lakini ni lazima kupata matokeo ili kuweza kutwaa ubingwa

Amesema mashabiki ni vyema wakafika uwanjani kuwaunga mkono wachezaji, wasisubiri ubingwa kwenye TV

"Ni Mechi ngumu kwelikweli kwa pande zote mbili,ingawa presha ipo kwetu lakini ili ushinde ubingwa lazima tupate matokeo kwenye mechi kama hizi," amesema

"Niseme nini zaidi ya kuwasihi sana mashabiki wetu wasituangushe leo, tuje kuujaza Uwanja ili tuwape nguvu wachezaji wetu.

"Tusisubirie ubingwa katikaTV pekee ,tusogee Uhuru jioni ili tuziweke hesabu katika daftari"

Katika michezo ya hivi karibuni ambayo Simba imecheza uwanja wa Uhuru, idadi ya mashabiki imekuwa ikipungua hali iliyomshangaza Manara, muhasishaji huyo namba moja wa Simba

Hata hivyo mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam zimekuwa kikwazo kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’