Aussems akosa wacheza wazawa wenye ubora

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 May 2019
Aussems akosa wacheza wazawa wenye ubora

Uongozi wa Simba huenda usifanye usajili mkubwa wa wachezaji wazawa baada ya kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems kupendekeza kuboresha mikataba ya wachezaji waliopo

Wakati msimu wa ligi ukielekea ukingoni, tayari michakato ya usajili imeanza na Simba imepanga kuimarisha kikosi chake

Hata hivyo imeelezwa wachezaji wapya watakosajiliwa na Simba wanapaswa kuwa na viwango vikubwa zaidi ya waliopo.

Kutokana na kigezo hicho, Aussems ameona ni bora kuboresha mikataba ya wachezaji wazawa alionao kwani nje ya Simba hakuona wachezaji wazuri zaidi yao

Hivi karibuni Aussems alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema kikosi chake hakitakuwa na mabadiliko makubwa, atasajili wachezaji wanne ambao nafasi wanazocheza ni walinzi wawili, kiungo mmoja na mshambuliaji mmoja

Katika hatua nyingine, Simba imeanza mazungungumzo ya kuhuisha mikataba ya wachezaji wake waandamizi

Aishi Manula, Paschal Wawa, Shomari Kapombe, Said Ndemla, James Kotei, Erasto Nyoni, John Bocco, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi,Asante Kwasi, Haruna Niyonzima na Nicolas Gyan ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’