Uchovu umechangia kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 May 2019
Uchovu umechangia kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wemepoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar leo kutokana na changamoto mbalimbli likiwemo suala la uchovu kwa wachezaji wake

Aussems amesema wamecheza mechi nyingi ndani ya muda mfupi hivyo baadhi ya makosa yaliyofanywa na wachezaji wake yanasameheka

Nahodha Msaidizi Mohammed Hussein alijifunga bao pekee lililoipa Kagera Sugar ushindi wa bao 1-0

"Nawapongeza Kagera Sugar kwa kupata ushindi leo. Tulifanya makosa tukajifunga, tumepata nafasi kadhaa za kufunga tukashindwa kuzitumia, tumekubali matokeo ndio mpira," amesema

"Kikosi changu kinakabiliwa na uchovu pamoja na majeruhi ya baadhi ya wachezaji. Tunajitahidi kuwapa mapumziko wachezaji lakini sasa tunakabiliwa na changamoto nyingine ya mfungo wa Ramadhani, wachezaji wengine wamefunga"

"Kabla ya mchezo wa leo tumeshinda michezo 18 kati ya 19 tuliyocheza, kufungwa ni jambo la kawaida, nampongeza kocha wa Kagera Sugar kwa kushinda leo"

Licha ya kupoteza mchezo wa leo, Simba inahitaji kushinda michezo mitatu kati ya sita iliyobaki ili kutetea ubingwa

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’