Kampuni ya SportPesa kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na uongozi wa Simba wametangaza viingilio vya mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki kati ya Simba dhidi ya Sevilla utakaopigwa Alhamisi ya May 23 katika uwanja wa Taifa
Kiingilio cha chini cha mchezo huo Mzunguuko ni Tsh 5,000/- wakati majukwaa ya VIP B nia Tsh 15,000/-
Pia kutakuwa na tiketi za Platinum ambazo zitapatikana kwa Tsh 100,000/-
Tiketi zimeanza kuuzwa kupitia Selcom
Mchezo utapigwa saa moja usiku
Sevilla inayoshiriki ligi kuu ya Hispania, La Liga tayari imethibitisha ujio wake kupitia ujumbe uliotumwa na klabu hiyo jana
ADVERTISE HERE