Okwi ataja siri ya kurejesha makali yake ya ufungaji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 May 2019
Okwi ataja siri ya kurejesha makali yake ya ufungaji

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba Emmanuel Okwi jana alifunga mabao matatu sawa na Meddie Kagere na kuisaidia Simba kupata ushindi mnono wa mabao 8-1 dhidi ya Coastal Union

Hiyo ilikuwa hat-trik ya pili kwa Okwi msimu huu

Kwa siku za karibuni Okwi amekuwa katika kiwango bora cha kuzifumania nyavu, kwa wastani akifunga karibu kila mchezo

Okwi aliuanza msimu kwa kasi akifanikiwa kufunga mabao saba katika michezo ya mwanzoni mwa msimu

Hata hivyo baadae alijikuta akishindwa kuzifumania nyavu kwa karibu miezi mitatu hali iliyopelekea wakosoaji wake kupata la kuzungumza

Lakini tangu Simba iondoshwe hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Okwi amezaliwa upya na amekuwa akitupia mabao nyavuni kila anapojisikia

Okwi amefichua kilichomsaidia ni uvumilivu na ushirikiano anaoendelea kupata kutoka kwa wachezaji wenzake

"Wakati nilipokuwa sifungi sikukata tamaa, nilijua ni kipindi cha muda tu ambacho kitapita" amesema Okwi

"Wenzangu waliendelea kunipa moyo na kunihamasisha nijitume zaidi"

"Lakini jambo jema ni kuwa Simba haitegemei mchezaji mmoja. Kila anayepata nafasi anaweza kufunga ndio maana mimi nsipofunga wapo wengine watafunga, tunacheza kwa kushirikiana"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
46m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE β†’