Simba yapania kupanda kileleni TPL leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 May 2019
Simba yapania kupanda kileleni TPL leo

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo wako uwanja wa Uhuru wakipepetana na Coastal Union katika mchezo ambao matokeo ya ushindi yataihakikishia Simba kurejea rasmi kileleni mwa msimamo wa ligi

Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 78, inahitaji alama mbili tu kuweza kuongoza ligi na kuishusha Yanga kwenye nafasi ya pili

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo na wana matumaini makubwa ya kuondoka na alama zote tatu

Juzi kocha wa mabingwa hao watetezi Patrick Aussems alisema wanahitaji kushinda michezo yote mitano itakayopigwa uwanja wa Uhuru kuanzia leo ili kuweza kutwaa ubingwa mapema

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa leo na michezo mingine minne itakayopigwa katika uwanja huo ili kuwapa sapoti wachezaji kutekeleza lengo la kutetea ubingwa kabla kuikabili Sevilla May 23

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’