Niyonzima atahadharisha mechi zilizobaki Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 May 2019
Niyonzima atahadharisha mechi zilizobaki Simba

Kiungo fundi wa Simba Haruna Niyonzima 'Fabregas' amesema licha ya kikosi chao kuwa na nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo, wanahitaji kupambana ili kufanikisha malengo yao

Niyonzima amesema wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wapinzani wao kutokana na dhana iliyojengeka kuwa waamuzi wanawapendelea

"Tuna nafasi kubwa ya kuwa mabingwa msimu huu, lakini kwa kuwa tayari kuna dhana mbaya juu yetu inaenezwa kama tusipokuwa makini inaweza kutuathiri

"Kila mechi tunayopata ushindi lazima wapinzani  wetu walalamike kwa kudai waamuzi wanatupendelea hiki kitu ni kibaya na kinaweza kutuvurugia malengo.

"Kwa michezo yetu mitatu tuliocheza  unaona kabisa hakuna suala la kupendelewa kama inavyodaiwa, lakini ninachojua yanasemwa hayo ili kuwapa hofu waamuzi wanaotuchezesha na kuwajenga  wapinzani tunaokutana nao kuwa Simba ni timu ya kupendelewa hivyo hawawezi kushinda"amesema Niyonzima

"Kulingana na hali ilivyo lazima wachezaji, benchi la ufundi na viongozi tuwe makini kwa kuhakikisha tunakwepa hujuma zote zinazoandaliwa dhidi yetu ili kutimiza malengo ya ubingwa tuliyo  nayo"

Simba inafukuzia ubingwa wa pili mfululizo ambapo kesho Jumatano itashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Coastal Union

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’