Manara airejesha 'Do or Die' mechi tano za ligi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 May 2019
Manara airejesha 'Do or Die' mechi tano za ligi

Uongozi wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, umesema kuwa wanarejea kutumia kampeni yao ya 'Do or Die' ambayo waliitumia katika mechi za mashindano ya kimataifa za Ligi ya Mabingwa Afrika sasa imehamia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa ajili ya kusaka pointi 15

Mabingwa hao watetezi wenye pointi 78 baada ya kucheza mechi 30, wamebakiza michezo nane ili kumaliza msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2018/19 wakati vinara wa ligi hiyo, Yanga ambao wana pointi 80 wamebakiza michezo minne.

Endapo Simba itapata ushindi wa mechi tano kati ya hizo zilizosalia, itafikisha pointi 93 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki ligi hiyo msimu huu, wakati Yanga ikishinda michezo yake yote iliyosalia itafikisha pointi 92.

Akizungumza jana jijini, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa lengo la kutumia kampeni hiyo ni kuhakikisha wanavuna pointi hizo na kutetea ubingwa wa ligi hiyo ambao bado wanaushikilia.

Manara alisema kuwa ili waweze kutimiza malengo hayo, wanahitaji mashabiki wa timu hiyo wajitokeze kuishangilia timu yao kama walivyofanya katika michezo ya kimataifa ambayo walishiriki msimu huu.

"Tuna mechi tano mfululizo Dar es Salaam, pointi 15 za Dar es Salaam ni lazima tuzichukue, mikoani kuanzia Mwanza, Musoma, wametuunga mkono sana, mara nyingi sisi tumekuwa tukiujaza uwanja katika mechi za kimataifa, kampeni yetu ni kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi, tunawaomba Wana-Simba wajitokeze kwa wingi, katika mechi tano, tuanze Jumatano, kama tunaweza kuujaza Uwanja wa Taifa, hatushindwi kwenye Uwanja wa Uhuru ambao unaingiza watu 15,000 hadi 20,000. Tunahitaji tushinde, wala hatutajali matokeo ya Yanga," alisema Manara

Kiongozi huyo aliongeza kuwa kikosi chao kimerejea salama kutoka Mbeya na kitaanza mazoezi leo kwa ajili ya kuikaribisha Coastal Union kutoka jijini Tanga kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kesho.

Mechi nyingine zitakazofuata za Simba za ligi hiyo inayotoa mwakilishi wa Tanzania Bara katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ni dhidi ya Kagera Sugar itakayocheza Ijumaa, Azam FC (Mei 13), Mtibwa Sugar (Mei 16) na dhidi ya Ndanda FC kutoka Mtwara itakayochezwa Mei 19 mwaka huu, zote kwenye Uwanja wa Uhuru.

Simba ambayo msimu huu ilifika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Sevilla ya Hispania na itafunga pazia la Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa kuvaana na wenyeji, Mtibwa Sugar.

Kwa hisani ya Nipashe

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’