Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema licha ya timu yake jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City, waamuzi wa mchezo huo hawakutenda haki
Aussems alichukizwa na tukio la waamuzi kuinyima Simba penati ya wazi baada ya Emmanuel Okwi kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
"Tangu waamuzi waadhibiwe baada ya kutupa penati mbili mchezo dhidi ya KMC, wamekuwa hawatutendei haki. Ni kama wanaogopa kutupa penati licha ya wachezaji wetu kufanyiwa madhambi eneo la hatari," amesema
"Muhimu ni kuwa tumepata alama tatu tulizozihitaji na sasa tunajiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prisons"
Aidha Msemaji wa Simba Haji Manara leo atazungumza na waandishi wa habari wa mkoani Mbeya kuhusu mwenendo wa ligi na kufafanua baadhi ya mambo yanayoihusu timu hiyo