Simba yasaka alama tatu dhidi ya Mbeya City leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 May 2019
Simba yasaka alama tatu dhidi ya Mbeya City leo

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wako mkoani Mbeya ambapo leo watashuka dimba la Sokoine kuwakabili wenyeji wao Mbeya City

Simba inayoshika nafasi ya pili baada ya kujikusanyia alama 72, inahitaji ushindi katika michezo saba tu ili kuubakisha ubingwa Msimbazi

Msemaji wa Simba Haji Manara amesema wachezaji wa timu hiyo wako katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo

"Timu imewasili salama mkoani Mbeya tayari kwa mchezo. Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi lakini wachezaji wetu watapambana kuhakikisha tunaondoka na alama zote tatu," amesema

Katika mchezo wa leo, Simba itamkosa nahodha wake John Bocco ambaye aliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania

Wengine watakaokosekana ni Asante Kwasi, Paschal Wawa na Shomari Kapombe

Baada ya mchezo huo Simba itaendelea kubaki mkoani Mbeya ambapo keshokutwa May 05 itachuana na Tanzania Prisons

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’