Sevilla itawajengea wachezaji uzoefu wa Kimataifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 May 2019
Sevilla itawajengea wachezaji uzoefu wa Kimataifa

Mafanikio ya Simba kwenye michuano ya SportPesa Super Cup msimu huu yameipelekea mabingwa hao wa Tanzania Bara kuteuliwa kuivaa Sevilla katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki utakaopigwa May 23 jijini Dar es salaam

Uongozi wa Simba umesema mchezo huo ni fursa adimu kwa wachezaji wake kwani utawasaidia kuwajengea uzoefu wa Kimataifa

Aidha Simba imesema itautumia mchezo huo kuitangaza Tanzania Kimataifa kwani wanajua utafuatiliwa na mamilioni ya mashabiki wa soka duniani kwani utarushwa mbashara na runinga mbalimbali kote duniani

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema uteuzi huo ni sahihi kwa Simba kwani ukiachilia mbali mafanikio waliyopata kwenye michuano ya SportPesa ukilinganisha na timu nyingine za Tanzania, Simba iko kwenye kiwango cha juu zaidi kwa sasa hapa nchini

"Simba kwa sasa ipo katika kiwango cha juu na kucheza na Sevilla kutasaidia kujua viwango vya wachezaji wetu katika mechi za kimataifa,” amesema

"Mechi hii inaiweka Tanzania katika historia kubwa sana katika soka. Historia zinaonyesha kuwa miaka ya nyuma, timu mbalimbali kutoka nje ya mipaka ya Afrika zilikuja hapa Tanzania na kucheza na Yanga na Simba, miaka ya hivi karibuni hakukuwa na ujio huo zaidi ya mwaka 2017 ambapo SportPesa iliileta timu ya Everton na kucheza timu ya Gor Mahia ya Kenya"

Sevilla ni moja ya timu kongwe na maarufu nchini Hispania na barani Ulaya. Imewahi kutwaa taji la Europa kwa misimu mitatu mfululizo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’