Bao la Dilunga lawavuruga mashabiki Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Apr 2019
Bao la Dilunga lawavuruga mashabiki Yanga

Bao la dakika za lala salama lililowekwa kambani na kiungo Hassani Dilung 'HD' na kuihakikishia Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania, limewavuruga mashabiki wa Yanga ambao wanalalamikia dakika saba za nyongeza zilizoongezwa na mwamuzi Elie Sasie

Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiiombea 'dua mbaya' Simba isishinde michezo yake na pengine wao kuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa

Msemaji wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki hao waache kuingilia kazi za waamuzi

"Ni jambo la ajabu kusema Simba imependelewa kisa mchezo kuongezwa dakika saba. Dakika hufidiwa pale mwamuzi anapoona muda ulipotezwa isivyo uwanjani," amesema Manara

Aidha Manara amewakumbusha mashabiki wa timu hiyo kuwa hata wao walipocheza na Lipuli Fc na kukubali kipigo cha bao 1-0 mkoani Iringa, waliongezwa dakika saba

Hesabu za Simba zimeendelea kukaa vizuri kuelekea ubingwa wa pili mfululizo baada ya ushindi wa leo

Simba imefikisha alama 72 ikitofautiana na Yanga kwa alama tano tu huku mabingwa hao watetezi wakiwa na michezo mitano ya viporo

Simba iko katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’