Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa tuzo za MO SIMBA zilizoanzishwa msimu uliopita na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji 'Mo', zitatolewa mwishoni mwa msimu huu
Taarifa iliyotolewa mapema leo imesema tuzo za mwaka huu zitahusisha wachezaji na mashabiki wa Simba ambao juhudi zao zimesaidia kupatikana kwa mafanikio makubwa msimu huu
Tuzo za mwaka huu zitakuwa na vipengele 11 ambavyo ni Mchezaji Bora, Goli Bora, Golikipa Bora, Beki Bora, Kiungo Bora na Mshambuliaji Bora
Nyingine ni Mchezaji Bora Mwanamke, Mchezaji Bora Mdogo, Shabiki Bora, Tuzo ya Heshima na Mhamasishaji Bora katika mitandao ya kijamii

ADVERTISE HERE