Nahodha wa Simba John Bocco amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru leo wakati mabingwa hao wa Tanzania watakapokuwa wakipepetana na JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Bocco amesema hesabu zao ni kutetea ubingwa waliotwaa msimu uliopita hivyo wamejipanga kuondoka na alama zote tatu leo
Bocco aliyefunga mabao 14 kwenye ligi msimu huu, amesema anatambua JKT Tanzania ni timu nzuri lakini wao ni bora zaidi na kikubwa wanahitaji alama tatu
"Tumefanya maandalizi ya kutosha, wachezaji tuna ari kubwa hakuna kitakachotuzuia kuibuka na ushindi katika mchezo huo," amesema Bocco
Nae kocha msaidizi wa Simba, Denis Kitambi, amesema mipango yao ni kuona Simba inaendelea kupata matokeo mazuri msimu huu.
Kitambi amesema wameupa uzito mkubwa mchezo huo kwani ni muhimu kwao kushinda ili kujiongezea pointi tatu nyingine