Kampuni ya SportPesa na TFF kwa pamoja wamefikia makubaliano kuwa mabingwa wa Tanzania Bara Simba ndio watakaocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sevilla utakaopigwa May 23 kwenye dimba la Taifa
Afisa Habari wa Simba Haji Manara ameishukuru kampuni ya SportPesa kwa kuwapa fursa hiyo ya kucheza na moja ya timu bora za ligi kuu ya Hispania
Amesema Simba itafanya maandalizi kamambe kuhakikisha wanaiwakilisha vyema Tanzania katika mchezo huo
ADVERTISE HERE