Aussems anataka ushindi mechi zote zilizobaki

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Apr 2019
Aussems anataka ushindi mechi zote zilizobaki

Kikosi cha Simba tayari kimerejea jijini Dar es salaam baada ya kumaliza ratiba ya michezo ya kanda ya ziwa

Simba kesho Jumanne itashuka uwanja wa Uhuru kuikabili JKT Tanzania katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya Tanzania Bara

Kocha Mkuu wa mabingwa hao watetezi Patrick Aussems amesema licha ya timu yake kukusanya alama tisa kutoka kanda ya ziwa, bado kazi haijamalizika na wanahitaji kushinda michezo yote iliyobaki waweze kutetea ubingwa wao

Aidha Aussem amesema ushindani kwenye ligi umeongezeka katika kipindi hiki cha lala salama hivyo wanahitaji kupambana kila mara wanaposhuka dimbani

"Bado tuna kazi ya kufanya, mechi zote ni ngumu, ligi bado ina ushindani, hakuna mechi rahisi, kila timu inahitaji ushindi ndio maana hakuna anayekata tamaa mpaka filimbi ya mwisho inapopigwa, tunataka kushinda kila mechi iliyopo mbele, " amesema

Baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania kesho, kikosi cha Simba kitaelekea mkoani Mbeya ambako kitacheza michezo miwili dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons

Kimahesabu, Simba inahitaji kushinda michezo nane kati ya 11 iliyobaki ili kujihakikishia ubingwa bila ya kujali matokeo ya mpinzani wake Yanga ambaye leo huenda akadondosha pointi zaidi dhidi ya Azam Fc

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’