Niyonzima ataka maombi ili afunge, aikamia Stand United

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Oct 2017
Niyonzima ataka maombi ili afunge, aikamia Stand United
Kiungo Haruna Niyonzima amewaomba mashabiki Simba waendelee kumuombea dua ili aweze kurudi katika ubora wake wa kuzifumania nyavu.

Niyonzima amejiunga na Simba msimu huu akitokea kwa mahasimu wao, Yanga hajafanikiwa kufunga bao tangu kuanza kwa msimu, lakini amekuwa ni mchezaji anayependwa na kukubalika kwa mashabiki wa Simba.

"Nilikuwa katika kipindi kigumu kidogo cha kuzoeana na wachezaji wenzangu, lakini nafarijika sasa nimeanza kuzoea mazingira ndani ya Simba.

"Siku zote uwa naamini mimi ni mchezaji mzuri, lakini siwezi kuwa mzuri bila ushirikiano na wenzangu, hakuna mchezaji wa aina hiyo.

"Nimekuja Simba kufanya kazi, najua mashabiki wanatamani sana kuona 'makeke' yangu uwanjani, lakini wasiwe na wasiwasi siku si nyingi mambo yatakuwa mazuri," alisema mchezaji huyo ambaye aliondoka Yanga ikiwa bado inamhitaji.

Kiungo huyo aliyepewa jina la fundi alisema tayari amekwishaanza kuzoea upepo ndani ya Simba na kusisitiza kwamba siku si nyingi ataanza kufanya vizuri.

Akizungumzia mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Stand United, Niyonzima alisema hiyo ni mechi ambayo hawatakiwi kupoteza.

"Tuko vizuri, hiyo ni mechi ambayo hatutakiwi kupoteza, tunaomba Mwenyezi Mungu atuamshe salama siku hiyo tupambane kwa ushindi kwani tumejifua kwa ajili ya kupata matokeo," alisema kiungo huyo.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’