Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC hapo jana, kikosi cha Simba kimeondoka asubuhi ya Ijumaa hii kuelekea mkoani Mara kuifuata Biashara United
Simba itacheza na Biashara United kesho Jumamosi
Wakati huo huo kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema watayafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana dhidi ya KMC
Licha ya Simba kuibuka na ushindi, haikuwa katika kiwango chake kilichozoeleka uchovu ukitajwa kuwa sababu ya kucheza chini ya kiwango
Aussems amesema anatambua jana wachezaji wake hawakucheza vizuri lakini muhimu ni ushindi walioupata ambao umewapandisha hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi
Simba imekuwa ikicheza kila baada ya siku mbili hali inayopelekea wachezaji kuchoka licha ya mabadiliko ya mara kwa mara ya kikosi yanayofanywa na Aussems