Ushindi dhidi ya Alliance umetuongezea morali - Niyonzima

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Apr 2019
Ushindi dhidi ya Alliance umetuongezea morali - Niyonzima

Kiungo Haruna Niyinzima amesema ushindi wa mabao 2-0 waliopata jana dhidi ya Alliance Fc umewaongezea morali wachezaji na wataendelea kupambana ili kuhakikisha wanatetea ubingwa waliotwaa msimu uliopita

Niyonzima aliye katika kiwango bora, aliifungia Simba bao la kwanza na baadae Okwi kuongeza la pili katika kipindi cha pili

"Mchezo haukuwa rahisi hasa kutokana na matokeo tuliyopata kwenye mchezo uliopita, tulikuwa na presha ya kupata ushindi," amesema Niyonzima

"Tunashukuru tumefanikiwa kuondoka na alama zote tatu, matokeo haya yametuongezea morali ya kufanya vizuri kwenye michezo ijayo"

Akizungumzia ugumu wa ratiba, Niyonzima amesema Simba ilisajili wachezaji 30 hivyo anaamini wataweza kukabiliana na changamoto ya kucheza kila baada ya siku mbili au tatu

"Kocha alituambia atakuwa akifanya mabadiliko ya kikosi ili kuhakikisha kila mchezaji anahusika. Hii ndio faida ya kusajili wachezaji wengi"

"Najua haitakuwa kazi rahisi lakini naamini tutafanikiwa kutetea ubingwa"

Simba imebaki jijini Mwanza ambapo kesho itashuka tena kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikabili KMC

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
13h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
13h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
16h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’