Tunahitaji ushindi dhidi ya Alliance Fc - Mkude

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Apr 2019
Tunahitaji ushindi dhidi ya Alliance Fc - Mkude

Kiungo Jonas Mkude amesema wanafahamu hawana nafasi ya kufanya makosa zaidi kwani wanahitaji kutetea ubingwa waliotwaa msimu uliopita

Simba iko mkoani Mwanza ambapo leo itachuana na Alliance Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba

Akizungumza baada ya mazoezi ya jana jioni, Mkude alisema baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, wanahitaji kupata matokeo dhidi ya Alliance Fc leo

"Hakuna mechi rahisi katika Ligi Kuu, lakini timu itakayokuwa na nidhamu uwanjani ndiyo yenye asilimia kubwa ya kupata pointi tatu muhimu. Tunahitaji kuwa kwenye ubora wetu ili tuweze kushinda kesho (leo)" amesema

Aidha, Mkude alisema hakuna timu inayoingia uwanjani kwa ajili ya kufungwa, ila anayeruhusu kufanya makosa ndiyo yanaweza kuwagharimu na hatimaye kupoteza mchezo.

"Tumekuja kupambana, mechi zetu hizi zimekuwa zinatizamwa sana na wapinzani wetu, tukifanya vizuri itatusaidia kutetea ubingwa tunaoushikilia na hiyo ndiyo mipango yetu"

Baada ya mechi ya leo, Simba itaendelea kubaki jijini Mwanza kusubiri mchezo dhidi ya KMC FC utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba pia.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’