Nyota kibao Simba kumaliza mikataba mwishoni mwa msimu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Apr 2019
Nyota kibao Simba kumaliza mikataba mwishoni mwa msimu

Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba imemuagiza kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems kuwasilisha ripoti yake kwa ajili ya usajili wa msimu ujao

Simba imedhamiria kuanza mapema maboresho ya kikosi chake ambapo imebainika mikataba ya nyota zaidi ya 10 inamalizika mwishoni mwa msimu

Baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukiongoni ni pamoja na John Bocco, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Paschal Wawa, Paul Bukaba, James Kotei, Asante Kwasi na Nicolas Gyan

Imeelezwa hatma ya wachezaji hao inasubiri mapendekezo ya Aussems ambaye ndiye aliyeachiwa jukumu zima la usajili huku uongozi wa Simba ukibaki katika utekelezaji

Hata hivyo idadi kubwa ya wachezaji hao wataendelea kubaki Msimbazi kutokana na mchango mkubwa waliotoa msimu huu

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema hawatarajii kukivuruga kikosi chao ambacho kimefanya vizuri msimu huu lakini watasikiliza kile kitakachopendekezwa na Aussems kwa ajili ya maboresho

"Masuala yote ya usajili Simba mwenye kauli ya mwisho ni kocha. Tunafahamu baadhi ya nyota wetu mikataba yao inamalizika, hata hivyo mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye kocha amesema tumuache, hivyo tutawapa mikataba mipya," amesema Magori

Baada ya Simba kuondoshwa hatua ya robo fainali michuano ya Ligi ya Mabingwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji 'MO' alisema msimu ujao wanataka kuwa na kikosi imara zaidi na hawatasita kuachana na wachezaji ambao mchango wao ni mdogo au watovu wa nidhamu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’