Simba yapewa tahadhari mchezo dhidi ya Alliance Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Apr 2019
Simba yapewa tahadhari mchezo dhidi ya Alliance Fc

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems kesho atakiongoza kikosi chake kuikabili Alliance Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba

Simba iliwasili jana jijini Mwanza na jioni ikafanya mazoezi. Leo inatarajiwa kujifua dimba la CCM Kirumba

Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 2-1, Simba haipaswi kupoteza alama zaidi. Matokeo ya ushindi ni muhimu kwa mabingwa hao watetezi

Mchezo mbovu ulioonyeshwa kwenye kipindi cha kwanza dhidi ya Kagera Sugar ndio ulioigharimu Simba, makosa hayo hayapaswi kurudiwa katika mchezo wa kesho

Aussems amesema wachezaji wake wanapaswa kucheza dakika 90 na sio dakika 45 kama walivyofanya mkoani Kagera juzi

Aidha Alliance Fc ya sasa sio ile ya mzunguuko wa kwanza ambayo Simba iliifumua mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Matokeo ya mchezo wa kwanza yasiwafanye wachezaji wa Simba 'wakawachukulia poa' wapinzani wao hao ambao wanashika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama 37

Kama ilivyokuwa kwa Kagera Sugar, timu ya Alliance Fc nayo iko katika vita ya kujinusuru isiteremke daraja

Watacheza kwa 'jihadi' kujaribu kupata matokeo hivyo ni mchezo ambao wachezaji wa Simba nao lazima wajitoe kwa dakika zote za mchezo ili kuondoka na alama tatu muhimu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’