Aussems ataja kilichoiponza Simba mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Apr 2019
Aussems ataja kilichoiponza Simba mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema timu yake haikucheza vizuri kwenye kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao Simba ilipoteza kwa mara ya pili msimu huu kwa kufungwa mabao 2-1

"Nawapongeza Kagera Sugar kwa sababu walikuwa na mchezo mzuri katika kipindi cha kwanza, sisi hatukuwa bora," alizungumza Aussems baada ya mchezo jana

"Walitumia udhaifu wetu kuweza kufunga mabao mawili ambayo kwetu haikuwa rahisi kuyarejesha yote kwenye kipindi cha pili licha ya kurekebisha makosa tuliyofanya kwenye kipindi cha kwanza"

"Wachezaji wangu walicheza dakika 45 za kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga bao moja na kutengeneza nafasi nyingine ambao tulishindwa kuzitumia. Hata hivyo mchezo ni dakika 90"

Baada ya mapumziko ya Pasaka, Simba itaelekea mkoani Mwanza kuikabili Alliance Fc kwenye mchezo mwingine wa ligi utakaopigwa keshokutwa April 23 katika dimba la CCM Kirumba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’