Zanzibar Heroes imeanza vizuri michuano ya Challenge baada ya kuilaza Rwanda mabao 3-1 katika mchezo wa mapema leo uliopigwa kwenye uwanja wa Kenyatta, Machakos nchini Kenya.
Ikicheza kandanda safi la kushambulia, Zanzibar Heroes ilijipatia mabao yake kupitia kwa Mudathir Yahya, Mohamed Juma na Kassim Khamis.
Zanzibar Heroes itarejea uwanjani keshokutwa Disemba 07 kumenyana na ndugu zao Tanzania Bara, kabla ya kumenyana na Kenya Desemba 9 na kukamilisha mechi zake za Kundi A kwa kucheza na Libya Desemba 11 huko huko Machakos.
Mchezo huo dhidi ya Tanzania Bara unatarajiwa kuwa mkali kwa kuwa unawakutanisha wachezaji wanaofahamiana vizuri.
Kikosi cha Zanzibar Heroes kimesheheni wachezaji wengi wanaokipiga katika ligi kuu ya Vodacom wengi wakitokea kwenye vilabu vya Yanga, Azam FC, Singida United, Mbeya City na Majimaji.

ADVERTISE HERE