Kagere ajivunia mafanikio Simba, aahidi ubingwa ligi kuu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Apr 2019
Kagere ajivunia mafanikio Simba, aahidi ubingwa ligi kuu

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amehamishia hasira zake katika Ligi Kuu baada ya klabu yake kuondolewa katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ilitolewa na TP Mazembe kwa jumla ya mabao 4-1 na kukatisha safari yao ya kuendelea kuwepo katika mashindano hayo na kugeukia katika Ligi Kuu.

Kagere alisema yaliyotokea katika Ligi ya Mabingwa ni historia na hivi sasa akili yao wameigeuzia katika Ligi Kuu kuhakikisha wanamalizia kile ambacho walikibakiza.

"Tulichokipata katika Ligi ya Mabingwa hivi sasa ni historia tayari, kikubwa hivi sasa tunachokiangalia ni Ligi Kuu, tunapambana kuhakikisha tunachukua ubingwa," alisema mshambuliaji huyo mwenye magoli 16 sawa na Salum Aiyee wa Mwadui Fc.

Kagere aliongeza kwamba licha ya kutolewa katika hatua ya robo fainali na Mazembe, anaimani wamefanikiwa kupata kitu kikubwa na wanajipanga kwaajili ya msimu ujao.

"Nina furaha ya kuwa katika kikosi kilichopambana muda wote katika Ligi ya Mabingwa, nawapongeza wachezaji wenzangu na benchi la ufundi pamoja na bosi wetu ‘Mo’, inabidi tujipongeze kwa hapa tulipofika," alisema.

Kagere amekuwa na kiwango kizuri tangu alipojiunga na Simba msimu huu baada ya kufanikiwa kufunga mabao 29 katika mashindano yote aliyoshiriki baada ya kufunga 16 katika Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa 6, Kagame Cup 4, Mapinduzi Cup 2 na Ngao ya Jamii 1.

MWANASPOTI

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
5h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
23h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’