Kagera Sugar vs Simba, mchezo wa kisasi leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Apr 2019
Kagera Sugar vs Simba, mchezo wa kisasi leo

Simba mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara, leo Jumamosi saa kumi kamili jioni watashuka kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera kuikabili Kagera Sugar katika mchezo muhimu kwa kila timu

Wakati Simba ikihitaji alama tatu kuendelea kusogea kileleni katika mpango wake wa kutetea ubingwa, Kagera Sugar iko katika hatari ya kuteremka daraja

Lakini pia, ukiachana na mazingira hayo, kwa misimu miwili iliyopita, Kagera Sugar ilihusika katika kuvuruga mipango ya Simba

Msimu wa 2016/17 Kagera Sugar iliisababishia Simba isitwae ubingwa baada ya kunyan'ganywa alama tatu ambazo walikuwa wamepewa awali na Bodi ya Ligi kufuatia Kagera Sugar kumchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi tatu za njano katika mchezo ambao Kagera Sugar ilishinda 2-1

Tukio hilo lilisababisha uongozi wa Simba kupeleka malalamiko FIFA, malalamiko ambayo yalitupiliwa mbali

Aidha mwaka jana wakati Simba ikiwa tayari imetangaza ubingwa, Kagera Sugar ikatibua tena siku muhimu kwa mabingwa hao ambayo walikuwa wakikabidhiwa kombe na Rais Dk John Magufuli kwa kuwachapa bao 1-0 kwenye uwanja wa Taifa

Kagera Sugar ndiyo timu pekee iliyopata ushindi dhidi ya Simba msimu uliopita

Msimu huu Simba imejipambanua kwa kuwa na kikosi bora zaidi ikiwa imeshinda michezo yote 11 iliyopita kwenye ligi na kuweka rekodi mpya

Ushindi katika mchezo wa leo utakuwa wa 12

Kocha Patrick Aussems amesema vijana wake wako tayari kuelekea mchezo huo na wamedhamiria kuondoka na alama zote tatu kama walivyofanya katika michezo 11 iliyopita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
4h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
4h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
7h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’