Ratiba haiwezi kutukosesha ubingwa - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Apr 2019
Ratiba haiwezi kutukosesha ubingwa - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamedhamiria kutetea ubingwa wa ligi kuu walioutwaa msimu uliopita hivyo wako tayari kukabiliana na ratiba ngumu ya viporo waliyopangiwa na Bodi ya Ligi

Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 juzi dhidi ya Coastal Union, kesho Jumamosi Simba itashuka tena uwanjani kumenyana na Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa dimba la Kaitaba mkoani Kagera

Simba imewasili Bukoba mapema leo tayari kwa mchezo huo

Aussems amekosoa mpangilio wa ratiba ikiwemo kupangiwa kucheza saa nane mchana. Hata hivyo amesisitiza kuwa kikosi chake kiko tayari hata wakipangiwa kucheza saa nne asubuhi

"Tumetoka katika kibarua kigumu cha michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tumekuja kwenye kazi ngumu ya kutetea ubingwa wetu. Tutakabiliana na ratiba tuliyopangiwa hata tukitakiwa kucheza saa nne asubuhi" amesema

"Kuchukua ubingwa si jambo la kuzungumza kwa mdomo, bali linahitaji matendo yenye uthubutu, ikiwa ni pamoja na mipango yake ndani ya kikosi"

Simba inakabiliwa kucheza michezo minne kanda ya ziwa dhidi ya Kagera Sugar, KMC, Alliance Fc na Biashara United kabla ya kuelekea mkoani Mbeya kuzikabili Tanzania Prisons na Mbeya City

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
17h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
17h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
20h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’