Wapinzani wa Simba katika mbio za ubingwa Yanga na Azam Fc zinaelekea kuishiwa pumzi mapema baada ya zote kupoteza michezo yao ya ligi iliyopigwa jana na leo
Baada ya hapo jana Yanga kuchapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar, leo Azam Fc nayo imechapwa bao 1-0 na Ndanda FC
Simba jana iliichapa Coastal Union mabao 2-1 na kufikisha alama 60
Simba inahitaji kushinda michezo miwili tu ili iweze kuipiku Azam Fc kwenye nafasi ya pili wakati ushindi katika michezo mitano ijayo itaihakikishia Simba kuiondoa Yanga kileleni
Simba ina michezo tisa ya viporo
ADVERTISE HERE