Wawa kuanza mazoezi Jumatatu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Apr 2019
Wawa kuanza mazoezi Jumatatu

Beki wa kati wa kimataifa wa Simba, Paschal Wawa, anatarajia kuanza mazoezi mepesi Jumatatu baada ya maumivu ya misuli aliyokuwa nayo kupona, imeelezwa.

Kutokana na maumivu hayo, Wawa ambaye amekuwa katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba aliukosa mchezo wa marudiano uliochezwa mjini Lubumbashi na pia jana dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa.

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, ameliambia Nipashe kuwa hali ya beki huyo imeimarika baada ya kupumzika katika muda aliopewa na daktari wao.

Rweyemamu alisema pia beki wao mwingine, Juurko Murshid na kiungo James Kotei wanaendelea vema, lakini hana uhakika kama watajumuishwa katika safari ya kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa.

"Kocha Mkuu (Patrick Aussems) ndiye ataamua kama wote tutakwenda Kanda ya Ziwa, lakini ni baada ya kupata majibu kutoka kwa daktari wa timu kuhusu maendeleo yao," alisema meneja huyo

Baada ya mechi ya jana, Simba inarejea jijini Dar es Salaam kuanza kujiandaa na safari ya kuifuata Kagera Sugar ambao watakutana Jumamosi kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’