Wanachama Simba kujazwa mapesa ya 'MO'

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
5 Dec 2017
Wanachama Simba kujazwa mapesa ya 'MO'
Wanachama wa Simba wana kila sababu ya kuchekelea mabadiliko mapya ya mfumo wa uendeshaji wa klabu yao, hiyo ni baada ya neema nzito kuwaangukia.

Wanachama hai wa Wekundu wa Msimbazi wameangukiwa na neema hiyo ambapo sasa watapewa hisa zenye thamani ya Sh4 bilioni wagawane, ikiwa ni ujira wao kwa kuitumikia timu hiyo ya Msimbazi kwa muda mrefu.

Juzi Jumapili, bilionea Mohammed ‘MO’ Dewji alitangazwa kuwa mshindi wa zabuni ya kuwekeza klabuni hapo ambapo atachukua asilimia 50 ya hisa kwa Sh20 bilioni, japo serikali imesisitiza kwamba mwekezaji hapaswi kuwa na zaidi ya asilimia 49 ya hisa za klabu.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya mgawo wa hisa hizo, wanachama wanapewa asilimia 10 ambazo watagawana. Hisa hizo zina thamani ya Sh4 bilioni.

Hisa nyingine asilimia 40 zenye thamani ya Sh16 bilioni zinabaki kama akiba kwa ajili ya kuuzwa baadaye.

Mjumbe wa Kamati ya Mabadiliko Simba, Mulamu Nghambi, alisema watahakiki wa wanachama kuwafahamu wanaostahili kupata mgawo.

“Unajua kuna wengine hawajalipa ada zao kwa muda mrefu, Katiba inasema asiyelipa kwa miezi sita mfululizo amekoma uanachama, tutawafahamu walio hai,” alisema.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
56m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE →
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
22h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE →