Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wameendelea kutafuna 'viporo' kuelekea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuifumua Coastal Union mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa dimba la Mkwakwani mkoani Tanga
Licha ya Coastal Union kutangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya kwanza, Simba ilitumia dakika 45 za kipindi cha pili kuondoka na alama zote tatu kupitia mabao mawili yaliyowekwa kimiani na Meddie Kagere 'MK14' kwenye dakika za 48' (p) na 68
Matokeo hayo yanaifanya Simba ifikishe alama 60, alama sita nyuma ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 66
Baada ya ushindi wa leo, Simba inaelekea mkoani Kagera ambapo April 20 itaumana na Kagera Sugar kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Kaitaba
ADVERTISE HERE