Bodi ya ligi kuu imefanya mabadiliko ya muda wa mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumatano kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mkoani Tanga
Mchezo huo ambao awali ulipangwa kupigwa saa kumi jioni, sasa utachezwa saa nane mchana
MKabadiliko hayo yamefanywa ili kuwapa nafasi mashabiki kushuhudia michuano ya AFCON U17 ambao kesho Tanzania itaumana na Uganda katika mchezo utakaopigwa dimba la Taifa saa kumi kamili jioni

ADVERTISE HERE