Mafanikio ligi ya mabingwa : Manara awashukuru mashabiki Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Apr 2019
Mafanikio ligi ya mabingwa : Manara awashukuru mashabiki Simba

Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa hamasa yao katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu huu

Ameyasema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kuondolewa na TP Mazembe katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-1, katika hatua ya robo fainali.

Manara amesema mashabiki na wanachama ndio walioisaidia kwa kiasi kikubwa Simba kufikia hatua hiyo, kwani waliisaidia Simba kushinda mechi tano za nyumbani.

"Mimi niseme kwa uwazi kabisa, nyuma ya mafanikio haya ni wanachama na mashabiki, bila ya wao kutusaidia tusingeweza kufika hapa. Wametupa nguvu ya dua na sapoti kwani tumeshinda mechi tano za nyumbani bila kupoteza", amesema Manara.

Aidha Manara amesema kuwa mipango yao msimu ujao ni kuvuka hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika kwa kuwa anaamini Simba wataibuka mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

EATV

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
47m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’